Tantrade: Watanzania changamkieni fursa India

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara nchini (Tantrade) imewataka watanzania kuchangia fursa zilizopo nchini India hususani katika jimbo la Haryana

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade, Latifa Khamis, kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba 2023) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku maalumu ya  watu wa India kwa jimbo la Haryana.

Amesema, jimbo la Haryana linaongoza katika uchumi wa India katika sekta ya Kilimo, Tehama, Madini na Viwanda.

“Watanzania tunatakiwa kujua fursa zilizopo tupo tayari kushirikiana na jimbo la Haryana tukaona tutumie fursa walizo nazo katika maonesho ili badae tufanye nao biashara yenye mikataba mikubwa yenye manufaa baina yetu,”amesena

Amesema Julai 12 mwaka huu wana siku maalum ya Zanzibar watahitimisha kutakuwa na promosheni ya uchumi wa buluu  na fursa zinazopatika watajulishwa washiriki wa ndani na wanje ya nchi.

Amesema, wameamua  kuja  na siku hizo maalumu  kwa sababu  wameangalia fursa zilizopo  katika maeneo mbalimbali ili washiriki wazijue.

Aidha, amesema katika siku hiyo maalumu waliambatana na msafara uliowakutanisha zaidi ya wadau 50 na viongozi wa jimbo hilo lengo likiwa ni  kuwaonyesha watanzania fursa zilizopo India.

Latifa, amesema wana mikataba ya manufaa baina ya Tanzania na India, hivyo serikali na jimbo hilo wapo kwenye maonyesho kuhakikisha kila mmoja anaondoka na fursa mbalimbali.

Amesema, wanatarajia kufanya tathimini ya maonyesho hayo ifikapo mwisho wa maonyesho ili kujiandaa na maonyesho mengine.

Naye Katibu Mkuu wa Serikali ya Haryana Makazi kwa Wote Idara ya Ushirikiano wa Nje, Dk. Raja Vundru, amesema wataendelea kushirikiana naTanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara na sekta ya madini.

“Nchi hizi mbili zina ushirikiano mzuri katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara kwani kuna bidhaa za Tanzania zinapatikana India kama parachichi ngano lakini pia bidhaa za India zinapatikana Tanzania huo ni uhusiano mzuri,” amesema Dk Vundru.

Habari Zifananazo

Back to top button