Tanzania: Chanjo ya polio kufikia watoto milioni 12.38

WAZIRI wa Afya ,Ummy Mwalimu amesema awamu ya tatu ya chanjo ya polio inalenga kuwafikia Watoto 12,386,854 wenye umri chini ya miaka mitano.

Ummy ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya zote nchini kupitia Kamati za Afya msingi za Mikoa na Halmashauri kusimamia kampeni ya utoaji wa chanjo ya polio ili kumfikia kila mtoto popote alipo.

Amesema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha kila mtoto anapata kinga na kuzuia Ugonjwa huo usiingie nchini.

Kupitia taarifa yake leo kwa vyombo vya habari, Waziri Ummy amebainisha kuwa awamu ya kwanza ilifanyika kuanzia Machi 24 hadi 27, 2022 na ilitekelezwa katika mikoa minne inayopakana na nchi ya Malawi ambayo ni Mbeya, Songwe, Njombe na Ruvuma.

“Kampeni hii ililenga kuwafikia watoto 975,839 wenye umri chini ya miaka mitano, na kufanikiwa kuwafikia watoto
1,130,261 sawa na asilimia 115 ya walengwa wote.

Amesema kuwa Awamu ya pili ya Kampeni hii ilifanyika nchi nzima kuanzia Mei18 hadi 21, 2022 ikilenga kuwafikia Watoto 10,295,316 wenye umri chini ya miaka mitano, na kufanikiwa kuwafikia watoto 12,131,049 sawa na asilimia 117.8 ya walengwa wote.

Ummy pia ametoa wito kwa Wazazi/Walezi, Taasisi za Umma, Binafsi, Dini, Asasi za Kiraia, Wawakilishi wa makundi mbalimbali ya Kijamii, Vyombo vya Habari na wananchi kwa ujumla kushirikiana na Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais – TAMISEMI katika utekelezaji wa kampeni hiyo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
gahsg
gahsg
1 year ago

Majina ya IDARA NANI KAKOSEKANA – Kazi ya matajiri!?
mavula
dines
mabuma
robert
aloys
godfrey
marry
maganya
robiey
sanga
tibi
fred
haule
cheche
Milka
Magret
mwakanema

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x