Tanzania, China kushirikiana uzalishaji nishati

WAZIRI wa Nishati, January Makamba amesema kuwa Tanzania na China zimefikia makubaliano kushirikiana katika utekelezaji wa miradi ya uzalishaji wa nishati jadifu.

Makamba ameeleza hayo jijini Beijing nchini China alipofanya mahojiano na kituo cha Televisheni cha CGTN na kubainisha kuwa makubaliano hayo yapo chini ya mpango wa ‘Belt and Road Energy Partnership’.

Katika makubaliano hayo China imeahidi kutoa fursa za mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa Tanzania katika ubunifu na uzalishaji wa teknolojia za kutengeneza nishati hiyo.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button