Tanzania, Hungary kushirikiana sekta ya elimu

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema ushirikiano baina ya Tanzania na Hungary una matunda mengi katika sekta ya elimu na mataifa hayo yataendelea kushirikiana zaidi.

Rais samia ameyasema hayo leo Julai 18, 2023 ikulu ya Magogoni Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari katika  mapokezi ya Rais wa Hungary Katalin Novak na ziara ya Rais huyo nchini.

“Katika elimu Hungary wamekuwa washirika muhimu sana kwa Tanzania hususan katika elimu ya juu kwa pamoja tumeweza kuimarisha ushirikiano wetu na leo mmeshuhudia tukisaini makubaliano ya kuimarisha zaidi ushirikiano wetu katika sekta ya elimu.”

Advertisement

“Makubaliano haya yanakuja na mipango mipya ambayo wanafunzi kutoka Hungury watanufaika pia na ufadhili wa kuja Tanzania na kusoma katika vyuo vyetu ,kwa mwaka huu tutaanza kuwapokea watano wakati Hungary wao watapokea wanafunzi 30 na namba zitakuwa zikiongezeka.” amesema Rais Samia