Tanzania ina madaktari bingwa wazalendo 2,469, Bunge limeelezwa.
Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel ametoa kauli hiyo leo bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Angelina Malembeka aliyetaka kujua Tanzania ina madaktari bingwa wazalendo wa magonjwa ya binadamu wangapi na katika magonjwa gani.
“Hadi sasa Tanzania ina jumla ya madaktari bingwa wazalendo 2,469 ambao wamesajiliwa na Baraza la Madaktari Tanganyika wa fani mbalimbali za udaktari bingwa.
“Kati yao madaktari bingwa 2,098 wapo katika sekta ya umma na madaktari bingwa 371 wapo sekta binafsi. Mheshimiwa Spika, madaktari hawa wamegawanyika katika maeneo 24 ya ubingwa,” amesema Naibu Waziri.
Comments are closed.