Tanzania kidedea Mashindano ya TEHAMA China

SHENZHEN, China: VIJANA watatu wa Tanzania kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Ndaki ya ICT (CoICT) wameibuka washindi katika mashindano ya TEHAMA duniani ya Huawei yaliyofanyika Mei 23-26, 2024 Shenzhen, China.

Vijana hao ni Dickson Mram, Matimu Mahimbo na James Amos ambao wana ujuzi katika uhandisi wa kompyuta, IT na mawasiliano ya simu, waliambatana na Mhadhiri msaidizi kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Mhandisi Jumanne Ally walishiriki katika mashindano hayo yaliyowashindanisha wanafunzi zaidi ya 470 kutoka nchi 49 duniani.

SOMA: Nape: Miaka 3 ya Samia kuna mabadiliko mawasiliano

Advertisement

Kufuatia ushindi huo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amewapongeza kwa kueleza kuwa ushindi huu unaonesha uwezo uliopo miongoni mwa vijana wetu wa kitanzania katika fani muhimu za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Vijana hao watarudi Tanzania kesho Mei 28, 2024 na wanawatarajiwa kupokelewa kwa shangwe na kupongezwa kwa kuwa mfano wa kuigwa na  vijana wengine wa kitanzania.

Waziri Nape ameuzungumzia ushindi huo kuwa mwanzo mzuri wa kujenga taifa lenye ubunifu katika fani za TEHAMA.

Waziri Nape ameongozana na Naibu Katibu Mkuu, Nicholaus Mkapa na ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Dunia wa Jumuiya ya Habari (WSIS) kwa mwaka 2024 (WSIS 2024) jijini Geneva, Uswisi kuanzia Mei 27 hadi 31, 2024.

Mkutano unaolengo kujadili masuala mbalimbali ya TEHAMA na uwezo wake katika kukuza maendeleo, kuimarisha upatikanaji wa habari na maarifa, kuchochea ustadi na kuhamasisha matumizi ya TEHAMA kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi..Mkutano huu unafanyika.

Ushiriki wa Tanzania kwenye mkutano huo ni moja ya jitihada katika kuimarisha mashirikiano yake duniani katika kukabili changamoto mbalimbali katika TEHAMA na kuongeza tija katika utekelezaji wa miradi ya TEHAMA.