Tanzania kinara kutoa fedha za utafiti

DAR ES SALAAM: TANZANIA ni nchi ya kwanza katika kutoa fedha za utafiti ikifuatia nchi ya Afrika Kusini katika nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk Amos Nungu ameeleza hayo katika kikao cha kujenga mahusiano mazuri na waandishi wa habari kilichoandaliwa na tume hiyo.

Dk Nungu alisema Tanzania imeonekana ya kwanza katika kusimamia na kuratibu utafiti, kikiwepo kutoa miongozo mbalimbali ya utafiti, kusimamia fedha na kuangalia tafiti zinazoweza kupelekwa kwa jamii.

Advertisement

“Kutokana na kusimamia vizuri wapo wanaotaka kujifunza Tanzania. Nchi ya Namibia wamesema watakuja kujifunza, Ghana pia kama watu wa nje wanaona haya, nao watakuja kujifunza,” amesema.

Naye Mkurugenzi wa Uratibu na Uendelezaji wa Utafiti COSTECH, Dk Bugwesa Katale alisema tume hiyo ni mwanachama wa mabaraza ya utafiti wa nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Amesema COSTECH imekuwa ikifadhili tafiti na bunifu mbalimbali ambazo zinatoa teknolojia chanya kwa taifa.

2 comments

Comments are closed.