Tanzania Kisiwa cha fursa, wawekezaji waimezea mate

MISRI: WAWEKEZAJI wa Kampuni ya Elsewedy Electric kutoka nchini Misri wamesema uwepo wa sera nzuri ya uwekezaji na ushirikiano mkubwa kutoka serikali ya Tanzania umewavutia kuwekeza nchini.

Aidha, Kampuni hiyo imezindua rasmi uwekezaji weye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani milioni 400 wa kongani ya viwanda 100 vinavyotarajiwa kujengwa eneo la Mlandizi, mkoani Pwani.

Akizungumza katika uzinduzi wa uwekezaji huo katika mkutano wa kimataifa wa wafanyabiashara uliofanyika mjini Cairo, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda wa Kampuni hiyo, Mohamed Alkaammah alisema uwekezaji wa kongani ya viwanda 100 ya kampuni hiyo inatarajia kuzalisha ajira zaidi ya 50,000 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.

Alisema uwekezaji huo ni matunda ya ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoifaya nchini Misri mwaka 2021 ambapo aliwahamasisha wawekezaji hao kuja kuwekeza nchini.

“Tunahaidi kushirikiana na Tanzania kuendelea kuwekeza na kufanya biashara na kuifanya kuwa kitovu cha viwanda Afrika,”alisema.

Kwa upande wake, Mkurungenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Gilead Teri alisema kuwa Tanzania imedhamiria kuendelea kushirikiana na wawekezaji kutoka Misri katika kuwekeza kwenye sekta mbalimbali.

Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara, soko na uwekezaji wake unakuwa kwa kasi kutokana muingiliano wa watu mbalimbali

“Tupo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na Sadc tuna jumla ya uhakika la soko la watu takribani 450 ambapo kwa upande wa miundombinu iliyopo nchini Tanzania ni ya uhakika ikiwemo reli pamoja na barabara,”alisema.

Rais wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Huru (GAFI) wa Misri, Hassan Heiba alisema uhusiano wa kiuwekezaji baina ya Misri na Tanzania umekuwa mfano wa kuigwa wa ushirikano wa nchi za Afrika kwenye suala zima la uwekezaji.

Alisema nchi za Afrika zinatakiwa kushirikiana kwa pamoja kukuza uchumi wa nchi zao kwa kufanya uwekezaji wa pamoja na kushirikiana na nchi nyingine.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Elsewedy Electric Afrika Mashariki, Ibrahim Oamar alisema kuwa katika uwekezaji wao ambao tayari wameshafanya nchini Tanzania ikiwemo kuwa miongoni mwa kampuni zinazojenga bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere na kiwanda cha uzalishaji wa vifaa vya umeme umekuwa na mafanikio makubwa hasa kwa kupata soko katika nchi za Afrika Mashariki na SADC.

Kongani ya viwanda 100 ya Elsewedy Electric ni miongoni mwa uwekezaji wa kimkakati ambao pia utatumia bandari kavu ya kwala na reli ya kisasa ya SGR kwa ajili ya kubebea mizigo.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Angila
Angila
23 days ago

I get paid more than 90$ to 400$ per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this I (Q)have earned easily $10k from this without having online working skills . Simply give it a shot on the accompanying site…
.
.
.
Here is I started.…………>> http://remarkableincome09.blogspot.com

Julia
Julia
23 days ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month I have earned and received $18,539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money Online.
.
.
Detail Here——————————————————–>>>  http://Www.BizWork1.Com

Joyceieves
Joyceieves
23 days ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 23 days ago by Joyceieves
Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x