WAKATI idadi ya Watanzania ni milioni 61.
74 pia kuna jumla ya majengo milioni 14.
3
Hayo yamesemwa na Rais Samia Suluhu Hassan, wakati akitangaza matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi, jijini Dodoma leo Oktoba 31,2022.
Rais Samia amesema, kati ya idadi hiyo ya majengo, Tanzania Bara kuna majengo milioni 13.9, wakati Zanzibar kuna majengo 440, 451.
“Kwa upande wa huduma za kijamii vituo vya afya ni 10,967 kati ya hivyo zahanati ni 7, 856 na vituo vya afya ni 1,490,” amesema Rais Samia na kuongeza kuwa kwa hospitali zipo 688.
Upanse wa elimu amesema zipo shule 25, 626, ambapo shule za msingi ni 19, 769 na sekondari ni 5,857.
“Idadi yetu Watanzania kwa mujibu wa sensa kama nilivyotaja, wito wangu kwetu sote na wadau wa maendeleo kutumia taarifa hii madhumuni yaliyokusudiwa ya kuboresha taarifa za Watanzania, “amesema.
Pia Rais Samia amezindua mwongozo wa Sensa ya Watu na Makazi, ili utumike katika kupanga maendeleo.
Muongozo huo ameukabidhi kwa viongozi mbalimbali, akiwemo Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi.