Tanzania kuokoa mabilioni kwenye viuatilifu

Matumizi holela viuatilifu yasababisha ugumba, saratani

DAR ES SALAAM: Tanzania iko mbioni kuokoa zaidi ya shilingi bilioni 4 zinazotumika kuagiza viuatilifu vya kilimo kutoka nje ya nchi baada ya kiwanda cha shirika la maendeleo nchini NDC kupitia kiwanda cha uzalishaji wa viuatilifu vya kibaiolojia kuanza uzalishaji wa viuatilifu hivyo.

Akizungumza wakati wanawake wa shirika hilo walipotembelea wakulima wa mboga mboga wa Mpiji Magohe Dar es Salaam kama sehemu ya shamra shamra za kuelekea siku ya wanawake duniani Kaimu mkurugenzi wa idara ya viwanda vya kuongeza thamani, Ester Mwaigomoli amesema Tanzania inaagiza viuatilifu hivyo kutoka nje jambo ambalo linaligharimu taifa fedha za kigeni.

Mtaalamu wa maabara kutoka kiwanda hicho kilicho chini ya NDC Jovin Magayane amesema serikali iliwekeza katika kiwanda hicho baada ya kuona zaidi ya 40% ya mazao yanayolimwa yanaharibika kutokana na wadudu dhurifu huku magonjwa ya mimea yakiigharimu serikali pesa nyingi.

Advertisement

Nao wananchi ambao ni wakulima wa mboga mboga wa eneo hilo wameishukuru NDC kwa kuwapatia suluhisho la kutotumia kemikali kuzalisha mboga hizo ili kuepusha madhara kwao na kwa walaji wa mboga hizo.