Tanzania kupata miradi uhifadhi mazingira

TANZANIA inatarajia kupata miradi ya uhifadhi mazingira na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo nishati jadidifu yenye thamani ya Sh trilioni 42.4.

Akizungumza jijini Dodoma leo Mei 11, 2023 Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk Switbert Mkama amesema miradi hiyo itasaidia kupunguza ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa.

Aidha, amesema miradi hiyo itafadhiliwa na Benki ya Dunia, Taasisi ya Afrika 50 na Shirika la Nishati la Afrika kwa kushirikiana na kampuni ya China Renewable Energies ambapo Kampuni ya Equinor iliahidi kukamilisha makubaliano ya mkataba wa ufadhili wa mradi wa gesi ifikapo Disemba 08, 2022.

Kutokana na Dk Mkama Fursa hiyo imekuja baada Rais Samia Suluhu Hassan kuwakutanisha marais watano kutoka Zambia, Zimbabwe, Malawi, Botswana, Makamu wa Rais wa Angola na watendaji kutoka Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika katika uzinduzi wa mtandao wa uzalishaji wa pamoja wa nishati jadidifu kwa nchi za kusini mwa Afrika na kujadili fursa za uwekezaji katika sekta hiyo na miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Akiendelea kutaja mafanikio ya mkutano huo, Dk Mkama amesema Kampuni ya TAQA ARABIA ya Misri imeahidi kujenga vituo 12 vya kusambaza gesi asilia kuanzia mwaka 2023 pamoja na kujenga uwezo wa vijana kuhusu teknolojia ya gesi katika vyombo vya usafiri.

“Mtakumbuka katika mkutano wa COP 27 Tanzania ilikuwa na banda lake ambalo uwepo wake umetoa fursa kubwa kwa Tanzania kujulikana na kupatikana kirahisi wakati wa mikutano ikiendelea. Hali ambayo iliwezesha kufanya majadiliano na kutoa ufafanuzi kuhusu fursa za uwekezaji na ushirikiano na vipaumbele vya nchi kuhusu hifadhi na usimamizi wa mazingira,“ amesema Dk Mkama

Aliendelea na kusema kuwa kuwa shirika la The Nature Conservancy (TNC) lipo tayari kuisaidia Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuanza biashara ya kuuza Hatifungani za Bluu (Blue Bond).

Itakumbukwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zitakazonufaika na programu ya uchumi wa bluu na kuhimili mabadiliko ya tabianchi katika bara la Afrika inayofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Serikali ya Norway imeahidi kuendelea kuisaidia Tanzania katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi, hususan utekelezaji wa Mchango wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (NDC).

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x