Tanzania, Malawi kushirikiana kuzalisha umeme

TANZANIA  na Malawi zimeingia makubaliano ya ushirikiano katika nishati, ikiwa kutekeleza agizo la wakuu wa nchi hizo mbili.

Akizungumza leo Agosti 11, 2023, Waziri wa Nishati January Makamba, amesema wameingia makubaliano hayo, ili kuimarisha sekta ya nishati katika nchi zote mbili na kuweka bayana makubaliano hayo.

“Makubaliano  yetu katika sekta ya nishati yanahusu maeneo matatu, kwanza kabisa kuzalisha umeme kwa pamoja kwenye mradi wa kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji katika mto Songwe.

“Ushirikiano katika utafutaji, utafiti  na uchimbaji wa pamoja wa gesi na mafuta na  kushirikiana katika ujenzi wa miundombinu ya umeme, “ amesema Waziri Makamba.

Makamba amesema makubaliano baina ya serikali hizo mbili yapo katika utaratibu maalumu, ambapo kutakuwa na  kamati ya pamoja ya mawaziri  na kamati ya wataalamu ya kufuatilia utekelezaji wa makubaliano hayo, ambapo kila nchi itateua wataalamu ndani ya mwezi mmoj,a huku vikao rasmi vinatarajiwa Oktoba mwaka huu.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati wa Malawi,  Ibrahim Matola amesema makubaliano hayo ni utekelezaji wa maagizo ya wakuu wa nchi hizo mara baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kufanya ziara nchini Malawi, lakini pia ziara ya Rais wa Malawi Lazarus Chakwera kutembelea Tanzania.

 

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button