Tanzania, Marekani kushirikiana teknolojia 5G

Samia aikaribisha Marekani uwekezaji maeneo matano

MAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amemhakikishia Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Marekani itashirikiana na Tanzania katika maendeleo ya teknolojia ya intaneti yenye kasi ya 5G ikiwa katika kujenga ushirikiano kati ya nchi hizo.

Kamala ameyasema hayo leo Machi 30, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya mazungumzo ya faragha na Rais Samia.

Pia ameahidi kusaidiana na Tanzania katika kukabiliana na uhalifu wa mitandaoni ambao sasa unashika kasi duniani kote.

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *