Tanzania mwenyeji mkutano wa chakula
MKUTANO wa Kimataifa wa chakula utaanza kesho Agosti 10 ambapo kampuni zaidi ya 500 zinatarajiwa kushiriki.
Mkutano huo umepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam, utaudhuriwa na wafanyabishara wa ndani na nje ya nchi, wakulima na wazalishaji bidhaa mbali mbali.
Akizungumza leo Agosti 9, 2023 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Pulses Ntwork (TPN) Zirack Andrew, amesema mkutano huo ni wa siku tatu na katika siku hizo kutakuwa na mabanda ya maonyesho ya aina tofauti tofauti ya mazao ya chakula kutoka katika kampuni mbalimbali hivyo kutakuwa kongamano na midahalo mbalimbali na maonyesho.
Amesema wanatarajia zaidi ya watu 3000 kutembelea mabanda kujifunza fursa zilizopo katika uzalishaji mazao ya chakula kupitia teknolijia ya juu kutoka nchi za nje hivyo ni vyema wakulima kuhudhuria ili kubadilishana uzoefu .
” Huu ni Mkutano unaofanyika kwa mara kwanza Afrika na mara ya kwanza Tanzania, vyama tofauti tofauti vya vyakula Afrika tumeshirikiana kuwaleta wenzetu toka India waliokuwa na uzoefu kufanya maonyesho kama haya kwa miaka mingi;…..: “Mashariki ya kati na sehemu nyingine tofaui tofauti Duniani ili kupata uzoefu na kuunganishwa na fursa ya kupata masoko ya kimataifa uuzaaji mazao ya chakula” amesema
Andrew amesema, dhima ya Mkutano huo kimsingi ni kufungua masoko ya mazao Afrika nzima na duniani kote.