Tanzania na India zimesaini hati 14 za Makubaliano

INDIA: Tanzania na India  zimetia saini hati za makubaliano 14 na mkataba mmoja, ambapo hati 10 zimehusisha taasisi za serikali na tano ni za sekta binafsi.

Hayo yamebainishwa Oktoba 9, 2023 katika ziara ya kikazi ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini India.

Mbali na kusaini hati hizo Rais Samia ameishukuru India kwa kuanzisha kampasi ya kwanza ya chuo cha IIT nje ya India chenye hadhi ya juu katika masuala ya teknolojia visiwani Zanzibar kitakachowanufaisha wanafunzi mbalimbali.

Advertisement

Masuala mengine yaliojadiliwa katika ziara ya Rais Samia ni pamoja na usalama wa mitandao, kushirikisha vijana hasa kupitia vyuo vya VETA, kutoa mafunzo kwa wahandisi wa madini, kushirikiana kwenye kilimo na miradi ya maji.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania na India zimekubaliana kukuza uhusiano wao wa kihistoria baina ya mataifa hayo mawili kwa kiwango cha ushirika wa Kimkakati.

 

 

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *