Tanzania, Uturuki kuendeleza sanaa

WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro Oktoba 27, 2023 akiwa jijini Dar es Salaam ameungana na raia wa Uturuki wanaoishi hapa nchini kusherehekea miaka 100 tangu kuanzishwa kwa taifa hilo.

Akizungumza katika hafla hiyo Dk Ndumbaro amesema Tanzania itendelea kushirikiana na nchi hiyo katika maeneo mbalimbali hususani kuendeleza Sanaa ya Tanzania hasa filamu ili ziweze kufika kiwango cha juu.

Hafla hiyo pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana, Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, mabalozi pamoja na viongozi wengine wa kidiplomasia.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button