TANZANIA imejiunga tena uanachama wa Shirikisho la Kimataifa la Mabaraza ya Sanaa na Mashirika ya Utamaduni (IFACCA) kupitia Baraza la Sanaa Taifa Basata.
Aidha, Katibu Mtendaji wa Basata, Kednon Mapana anakuwa mjumbe atakayeiwakilisha Tanzania katika mikutano ya Shirikisho la Kimataifa la Mabaraza ya Sanaa na Mashirika ya Utamaduni ambapo kwa mwaka huu yatafanyika nchini Sweden.
Taarifa iliyotolewa leo Machi 15, 2023 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo imeeleza kuwa hatua hiyo ni matokeo mazuri ya kuimarika diplomasia na ushirikiano wa kimataifa.
Katika taarifa hiyo, Waziri wa wizara hiyo, Pindi Chana ameipongeza Basata kwa kuwa mwanachama wa shirikisho hilo jambo litakalosaidia kukuwa kwa masuala mbalimbali ya wasanii wa Tanzania.