Tanzania yang’ara uwezeshwaji wanawake

DODOMA; TANZANA imepiga hatua katika uwezeshwaji wanawake ngazi za maamuzi, ambapo wanawake wengi wamepewa nafasi kuongoza sekta mbalimbali.

Akizungumzia kuhusu ongezeko hilo katika mahojiano maalum na Dailynews Digital, Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson, amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizopongezwa kimataifa kuhusu ongezeko kubwa la wanawake viongozi katika ngazi za maamuzi.

Amesema mafanikio hayo yametokana na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya usimamizi wa hayati Rais Dk John Magufuli, ambaye alianzisha safari hiyo na sasa Rais Dk Samia Suluhu Hassan anaiendeleza na kuifanya Tanzania kuwekwa nafasi nzuri ya uwezeshwaji wanawake ukilinganisha na mataifa mengine Afrika.

“ Tanzania tunafanya vizuri katika ngazi nyingi mfano uwakilishi wanawake duniani katika uchaguzi wa mwaka 2023, wastani wanawake walikuwa asilimia 26.9 lakini kwa Tanzania pekee wastani wa uwakilishi wanawake bungeni ni asilimia 37.4 maanake Tanzania tumepiga hatua tumezidi ule wastani nchi nyingine ambazo zina mapungufu wastani asilimia kumi,” amesema Dk Tulia.

 

Habari Zifananazo

Back to top button