Tanzania yapanda nafasi ya 6 kiuchumi

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba amesema Tanzania inasonga mbele licha ya nchi zote duniani kupita kwenye misukosuko ya kiuchumi ambapo uchumi wa nchi unatarajiwa kufikia dola za Marekani bilioni 85.6

Akiwasilisha bajeti ya serikali leo Juni 15, 2023, Mwigulu amesema kwa mujibu wa jarida la uchumi la Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) la Aprili 2023, uchumi wa Tanzania unatarajiwa kufikia dola za Marekani bilioni 85.4 mwaka 2023 kutoka dola bilioni 69.9 mwaka 2021.

Amesema Tanzania imepanda hadi nafasi ya sita ikilinganishwa na nchi nyingine Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiongozwa na nchi za Kenya 5 (dola bilioni 116.0), Ethiopia (dola bilioni 120.4), Angola (dola bilioni 121.4), Afrika Kusini (dola bilioni 405.7) na Nigeria (dola bilioni 477.4).

Nchi nyingine zenye uchumi mkubwa chini ya Tanzania ni Ghana (dola bilioni 72.8), Ivory Coast (dola bilioni 70.0), DRC (dola bilioni 62.8) na Uganda (dola bilioni 48.8).

“ Hivyo, watanzania tunapotoa mifano ya wapi tunaelekea tuyajue mataifa yalioko mbele yetu.”Amesema Mwigulu

Amesema, programu alizoanzisha na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, za kuwekeza kwenye sekta za uzalishaji na kukuza uwekezaji na uwezeshaji wananchi kiuchumi siku sio nyingi mataifa mengi tutayavuka.

Habari Zifananazo

Back to top button