Tanzania yapewa heko huduma za Mahakama

DAR ES SALAAM: Tanzania imepiga hatua kubwa katika shughuli za utoaji huduma za mahakama ikichagizwa na matumizi ya Tehama.

Kauli hiyo imetolewa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Elisante Ole Gabriel ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Watendaji wa Mahakama nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEAJAA)

Amesema nchi hizo zinajivunia hatua kubwa iliyopigwa na Tanzania katika utoaji haki.

Advertisement

Elisante ameyasema hayo leo katika kikao cha Kamati Kuu ya Watendaji wa Mahakama nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEAJAA) kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema mafanikio hayo ni matunda ya Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuweka mazingira wezeshi na rafiki ya uendeshaji wa shughuli hizo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Kamati hiyo Beuhardt Kukuri amesema wanafurahishwa na jinsi Tanzania ilivyoandaa mkutano huo huku akieleza kuwa wameridhika na jinsi shughuli za kutoa haki zinavyoendeshwa na kusisitiza ushirikiano zaidi kwa mataifa hayo.

Baada ya kuhitimisha kikao hicho wajumbe wote 13 wa kamati hiyo watatembelea vituo mbalimbali vya utalii ikiwemo safari ya kwenda kutalii Zanzibar.