Tanzania yapokea Sh trilioni 1 Global Fund

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imepokea msaada wa Sh trilioni 1.4 kutoka Global FUND ili kutekeleza afua mbalimbali za UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria nchini kote kwa malengo endelevu ya Milenia ambayo yanakusudiwa kufikiwa ifika mwaka 2030.

Upokeaji wa msaada huo umefanyika leo Januari 31, 2024 chini ya Waziri wa Fedha  Mwigulu Nchemba na Waziri wa Afya  Ummy Mwalimu kwa pamoja wameshuhudia utiji saini wa makabidhiano ya msaada huo baina ya Global Fund na Serikali ya Tanzania.

“Msaada huu wa fedha unalenga kutekeleza afua mbalimbali za UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria nchini kote lengo likiwa ni kutekeleza malengo endelevu ya Milenia ambayo yanakusudiwa kufikiwa ifika mwaka 2030″.
Amesema Waziri Ummy

Advertisement

Ummy amewashukuru Global Fund kwa msaada huo mkubwa katika Sekta ya Afya na kwa kuridhia ombi la Sekta ya Afya kutumia frdha za msaada kutoka Global Fund kwa ajili ya kusomesha na kuwaajiri wataalam wa afya ngazi ya jamii (Community Health Workers) wapatao 5,000  kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo ambapo wataalam hao watasaidia kuleta mabadiliko ya utoaji wa huduma za afya nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Global Fund katika sehemu ya High Impact Africa 2 Linden Morrison ameipongeza Tanzania kwa kushika nafasi ya nne kati ya nchi zinazopokea fedha hizo kutoka Global Fund.

“Lakini pia naipongeza Tanzania kwa kuendelea kutumia vizuri fedha hizo za msaada kutoka GLOBAL FUND ambapo Tanzania imefikia asilimia 92 ya utumiaji wa fedha hizo na hali hii inapelekea kuzifikia afua nyingi katika maeneo ya Kifua Kikuu, UKIMWI nà Malaria”. amesema

/* */