Tanzania yataka mbinu kukabili rushwa

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amezitaka nchi za Umoja wa Afrika (AU) kuangalia mbinu za kukabili rushwa. Abdulla alisema hayo jijini Arusha jana kwa niaba ya Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi katika uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Afrika yanayofikia kilele kesho.

“Tutumie nafasi hii kutathmini kiwango cha mapambano kilichochukuliwa na nchi zetu, tuangalie njia bora zaidi za kuendeleza mapambano ya rushwa kwa sababu rushwa ina madhara kwa wote,” alisema. Abdulla alisema Tanzania imepewa heshima ya kufanya maadhimisho hayo ikiwa miaka 20 tangu kusainiwa kwa mkataba wa kukabili rushwa barani Afrika.

Alisema msimamo wa serikali ni kuendelea kupambana na rushwa kwa sababu ni adui wa maendeleo na kuwataka wadau, taasisi,wananchi kila mmoja kwa nafasi yake lazima apambane na rushwa.

“Ni wajibu wetu kuikabili kwa ushirikiano na wengine, na ndio maana leo tuko hapa na watu wengine nje ya nchi, sote tukishikamana tutapunguza kiwango cha rushwa Afrika na itatuongezea sifa ya utawala bora,” alisema.

Awali Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Umoja wa Afrika ya Mapambano ya Rushwa, Paschal Antonio Joachim alisema matembezi ya amani yaliyofanyika jana Arusha ni muhimu yanaonesha dhahiri wanavyopambana na rushwa.

Joachim alisema madhara ya rushwa yanaonekana kwenye maendeleo hivyo ni lazima mapambano yafanywe kuipinga kuhakikisha inakoma. “Tumekusanyika kuadhimisha miaka 20 ya kupambana na rushwa yaliyoidhinishwa na wakuu wa nchi barani Afrika katika mkutano wa Maputo, Msumbiji.Hatua mbalimbali zimechukuliwa kwa wale wote wanaojihusisha na rushwa na safari hiyo inaendelea,tunataka Afrika iwe huru dhidi ya rushwa,’’ alisema Joachim.

Alisema pamoja na changamoto katika mapambano ya rushwa Afrika haijakata tamaa na wanaendelea kupambana na kutoa mwito kwa vijana ambao ni nguvukazi na agenda ya Afrika kuanza na kuendelea kupambana na rushwa ili kuijenga Afrika wanayoitaka.

Akizungumzia maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), Salum Hamduni alisema maadhimisho hayo ya siku tatu yalianza jana kwa kufanywa matembezi ya amani kupinga rushwa.

Maadhimisho hayo yanafanywa kwa kuendeshwa kongamano la wadau ambao watajadili uzoefu wa Afrika katika kupambana na rushwa.

Aidha, katika maadhimisho hayo Bodi ya Umoja wa Afrika Mapambano ya Rushwa watatoa mrejesho na pia Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar (ZAECA) na Takukuru nao watazungumzia uzoefu wao.

Pia elimu kuhusu maadili, utawala bora, uhujumu uchumi, jinsi ya kupambana na rushwa, madhara ya dawa za kulevya, na mabanda ya utalii yatakuwepo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, George Simbachawene akizungumza katika ufunguzi huo alisema bado elimu ya rushwa inahitajika kwa wananchi na kuwa serikali itaendelea kushirikiana na wadau katika vita hivyo.

Rais Samia Suluhu Hassan kesho anatarajiwa kuhitimisha kilele cha maadhimisho Arusha. Imeandikwa na Veronica Mheta (Arusha) na Ikunda Erick (Dar es Salaam).

mezitaka nchi za Umoja wa Afrika (AU) kuangalia mbinu za kukabili rushwa. Abdulla alisema hayo jijini Arusha jana kwa niaba ya Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi katika uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Afrika yanayofikia kilele kesho.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button