Tanzania, Zambia kujenga bomba la gesi

MAWAZIRI sita wa Nishati, Ulinzi na Mambo ya Ndani ya Nchi wa Tanzania na Zambia, wamekubaliana kuongeza nguvu ya ulinzi na usalama kwenye Bomba la Mafuta la Tanzania-Zambia (TAZAMA), ambalo sasa linasafi risha mafuta safi .

Aidha, alisema wamekubaliana pia kuanza ujenzi wa bomba la gesi kutoka Tanzania hadi Zambia.

Kauli hiyo imetolewa baada ya mkutano wa mawaziri hao wa Nishati, January Makamba, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni na kwa upande wa Zambia ni Waziri wa Ulinzi, Ambrose Lufuma, Waziri wa Nishati, Peter Kapala, Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Nchi, Jacob Mwiimbu.

Advertisement

Akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kikao hicho cha siku mbili kilichofanyika Dar es Salaam, January alisema hatua hiyo ya kuimarisha ulinzi imetokana na bomba hilo lililojengwa kuanzia Kigamboni, Dar es Salaam hadi Zambia katika miaka ya 1960 kuanza kutobolewa kutokana na kusafirisha mafuta masafi.

Awali lilikuwa linasafirisha mafuta ghafi. January alisema mwaka jana walifanya kikao cha kwanza kujadili suala hilo na kikao hicho ni cha pili na kuwa katika kikao hicho hicho wamekubaliana kupanua bomba hilo kutoka nchi nane za sasa hadi kufikia nchi 12 ili liweze kupitisha mafuta kutoka tani 800,000 za sasa hadi tani milioni 1.5.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Msafara kutoka Zambia na Waziri wa Ulinzi, Lufuma alisema kati ya maeneo waliyokubaliana kushirikiana ni pamoja na Polisi wa nchi zote mbili kuweka doria kwenye maeneo bomba hilo linakopita na kufunga kamera za kisasa kwa upande wa Tanzania na Zambia zikiwemo zilizowekwa kwenye ndege zisizokuwa na rubani.

2 comments

Comments are closed.