Tanzania,Morocco kwenda Pamoja katika michezo.

DAR ES SALAAM: Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Morocco hapa nchini Zakaria El Goumiri kuhusu ushirikiano baina ya Tanzania na Morocco katika Sekta ya Michezo.

Kikao hicho kimefanyika Septemba 13, 2023 katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salam ambapo Waziri Dk Ndumbaro amewasilisha salamu za pole kwa nchi hiyo kufuatia Tetemeko la Ardhi lililopita katika nchi hiyo na kumhakikisha Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
Kwa upande wake Balozi . Zakaria El Goumiri amepokea salamu za pole kutoka Tanzania, ambapo pia amesema nchi yake itaiunga mkono Tanzania katika ujenzi wa miondombinu ya michezo ili kuendelea kukuza vipaji vya wanamichezo ambao watakuwa ni hazina kwa mataifa hayo kwenye timu za taifa.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Saidi Yakubu ambaye amesema ushirikiano wa Tanzania na Morocco katika sekta ya michezo ni wa kihistoria na kila mara nchi hizo mbili zimekuwa na mechi za kirafiki katika nyakati tofauti na hivi karibuni timu moja kutoka nchi hiyo itakuja nchini kucheza na timu mojawapo.

Habari Zifananazo

Back to top button