TARI yashauri uwekezaji kwenye mabibo

TAASIS ya Utafiti wa Kilimo Nchini (TARI) kituo cha Naliendele imewaomba wadau wa zao la korosho na wawekezaji kutoka ndani na nje kuwekeza kwenye kilimo cha mikorosho ya mabibo ili kunufaika na faida ambazo zinapatikana kwenye mabibo.

Mtafiti na Maratibu wa Uhalishaji wa Teknolojia na Mahusiano kutoka TARI-Naliendele Bakari Kidunda amesema kilimo cha mikorosho ya matunda ya mabibo Kwa Tanzania bado hakijapewa kipaumbele licha ya kuwa na faida kubwa kulinganisha na kilimo cha korosho ghafi (korosho karanga).

“Ukilinganisha ukubwa wa faida ya korosho, uzito mkubwa au faida kubwa iko kwenye mabibo kuliko korosho karanga, ukichukua asilimia 100 ya korosho, asilimia 90 faida ipo kwenye bibo na ile korosho karanga ni asilimia 10 tu.” amesema.

Amesema kwa sasa wakulima wa korosho nchini wamejikita zaidi kwenye kilimo cha Korosho ghafi cha karanga ambapo wanatupa yale mabibo ambayo yanafaida kubwa.

Amesema mabibo hutumika katika kutengeneza bidhaa nyingi na za faida kubwa kama vile juice, piko, ethanol , waini na bidhaa nyingine nyingi.

“Pia matunda ya mabibo yana vitamin C mara tano zaidi ya matunda mengine ambapo ni faida kubwa kiafya,” amesema.

Kidunda amesema kwa sasa TARI-Naliendele wako kwenye mchakato wa kuainisha aina ya mabibo kwenye matumizi ya bidhaa kama vile juisi, waini, piko, ethanol na bidhaa zingine ili watu wakitaka kuwekeza wajue wanawekeza kwenye aina gani ya mabibo

Amesema yapo mabibo kwa ajili ya tunda ambalo linaliwa , mabibo kwa ajili ya Juisi, waini, na matumizi mengine.

Amesema nchi zingine ambazo zinalima korosho wana mikorosho kwa ajili ya kuzalisha matunda ya mabibo tu ambapo amesema kwa Tanzania bado soko la mabibo halijafahamika zaidi kwa sababu watu wengi wamejikita kwenye kilimo cha korosho karanga.

“Tungependa watu wawekezaji kwenye kilimo cha mikorosho ya mabibo, mbegu tunazo za kutosha na teknolojia, ipo na mafunzo ya namna ya kuendesha kilimo hicho tunatoa bure kwa wahitaji kwenye vituo vyetu vyote vya utafiti nchini.” amesema Kidunda.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button