TARURA: Ujenzi kwa teknolojia ya mawe huokoa gharama

WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), imesema ujenzi wa barabara na madaraja kwa kutumia teknolojia ya mawe na matofali huokoa gharama kwa asilimia 50.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma, Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff, alisema teknolojia hiyo hupunguza gharama kwa sababu hutumia marighafi ambazo zinapatikana katika maeneo husika

“Tumejenga madaraja ya mawe zaidi ya 73 Kigoma kwa sh bilioni 1.4, lakini pia ujenzi unaendelea katika Mikoa ya Mwanza, Iringa na Singida, ambapo bei ni nafuu na ukizingatia mawe yanapatikana katika maeneo mengi nchini,” amesema na kuongeza kuwa:

“Huu ni mkakati wetu, ambapo tunaangalia maeneo yote yenye mawe ambayo yatahusika katika ujenzi, ambapo kwa kushirikiana na wafadhili kutoka Ubelgiji, tunaanza kufundisha mafundi katika kujenga madaraja na sasa wapo Kigoma wanafanyiwa mafunzo na wakirudi katika maeneo yao nao wetafundisha wengine.”

Habari Zifananazo

Back to top button