Tasac yatahadharisha uchafuzi mazingira baharini

MAMLAKA  ya Udhibiti wa Usafiri kwa Njia ya Maji Nchini (TASAC) imevitaka vyombo vyote vinavyotoa huduma mbalimbali majini zikiwemo meli kutofanya uchafuzi wowote wa mazingira kwenye maeneo hayo kinyume na hapo hatua za sheria zitachukuliwa.

Akizungumza leo mkoani Mtwara, Mkurugenzi wa Ulinzi, Usalama na Utunzaji wa Usafiri Majini wa mamlaka hiyo Leticia Mutaki amesema katika maeneo hayo wanaangalia uchafuzi wa mazingira unaotoka kwenye meli ikiwemo umwagaji wa mafuta kwenye bahari na endapo itabainika kuwepo kwa tukio hilo hatua za kisheria zitachukuliwa.

‘’Kwahiyo tunaangalia meli isimwage uchafu, mafuta baharini lakini pia tunaangalia hata meli ambazo zinaweza zikafanya vitendo vyovyote vile kinyume na sheria hivyo kama kuna meli tutaiona kutokana na mfumo na vyombo vyetu tulivonavyo kama inafanya nini…. tutachukua hatua kwa kushirikiana na vyombo vyetu vingine vya serikali.’’amesema Mutaki.

Amesema jukumu lingine  kubwa la mamlaka ikiwa ni pamoja na kuhakikisha vyombo  hivyo vyote viko salama na vinapokuwa vimetimiza masharti ya ubora na usalama vinapatiwa leseni kwa ajili yakuendelea kutoa huduma za usafirishaji wa mizigo pamoja na abiria kwenye maeneo hayo.

Amesema  lengo la kuja mkoani humo ikiwa ni pamoja na kukagua shughuli mbalimbali za udhibiti ambapo wao kama mamlaka wanahakikisha vyombo vyote vinavyotoa huduma  baharini vinakuwa na ubora na usalama wa uhakika kuweza kutoa huduma kwenye eneo hilo ili kuepukana na majanga mbalimbali ikiwemo ajali zinazoweza kutokea baharini kupitia vyombo hivyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Tasac, Nahodha Mussa Mandia amezungumzia umuhimu wa kuwepo kwa mnara wa mawasiliano wa kisasa katika mkoa huo utaosaidia taarifa zisifuje ambazo hazikustahili kuvuja, kwasababu usalama na ulinzi wa habari siyo kila kitu kinapelekwa kwa watu/wananchi bali kinatakiwa kiende kwenye vyombo maalum.

‘’Katika mawasiliano kuna mawasiliano ambayo ni ‘public’ na kuna mawasiliano ambayo yanatakiwa yaende kwenye vyombo maalum kwahiyo kutokuwa na manara wa kisasa hapa maana yake taarifa zinaweza zikavuja ambazo hazistahili kuvuja,   changamoto iliyopo ni kwamba uliyopo ni wa muda mrefu miundombinu yake ni chakavu’’amesema Mandia

Mamalaka hiyo ipo ziarani mkoani humo na kupata fursa ya kutembelea baadhi ya maeneo ikiwemo mamalaka ya usimamizi wa bandari (TPA) mkoani Mtwara, kivuko cha MV Kitunda, mnara wa mawasiliano wa mkoa wa mtwara utakaosaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa mwambao wa pwani, eneo la mawasiliano baina ya mamiliki wa meli pamoja na Tpa linalomilikwa na mamaka hiyo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Angila
Angila
27 days ago

I have just received my 3rd paycheck which said that $16285 that i have made just in one month by working online over my laptop. This job is amazing and its regular earnings are much better than my regular office job. Join this job now and start making money online easily by
.
.
.
.
Just Use This Link……..> > > http://Www.Smartcareer1.com

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x