Tasac yatoa mafunzo Mara

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeanza kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa sheria mkoani Mara ikiwa ni mkakati wa kujua mabadiliko ya sheria mbalimbali za shirika hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, DK Khalfan Haule amefungua mafunzo hayo na kusisitiza umuhimu wa kujua mabadiliko hayo   ili kutekeleza majukumu ya usimamizi wa sheria, usalama wa wananchi na vyombo vya usafiri majini.

Ofisa Mfawidhi Tasac Mkoa wa Mara na Simiyu, Abed Mwanga amesema zamani vivuko hivyo vilikuwa chini ya sheria ya Sumatra, lakini kwasasa vitasimamiwa na Tasac kwa mujibu wa sheria na itaendelea kutoa mafunzo hayo kwa wadau mbalimbali.

Habari Zifananazo

Back to top button