TASAC yawaondoa hofu wadau wa Bandari

DAR ES SALAAM :SHIRIKA la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC) limesema changamoto ndogondogo zinazolalamikiwa na wadau wa mbalimbali wa bandari zinaendelea kushughulikiwa ili kuhakikisha ufanisi unaongezeka maradufu na hivyo kuharakisha ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa TASAC, Mohamed Salum wakati akizungumza katika Kikao cha wadau wa bandari waliokutana jijini Dar es salaam kujadili changamoto zinazo lalamikiwa na wadau wa Bandari ambazo ni pamoja na mifumo ya uendeshaji, Scana za mizigo, Tozo, miundombinu na matumizi ya dola kwa mizigo na namna ya kuzitatua.

Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es salaam Mrisho Mrisho amesema bandari inajipanga kuongeza matumizi ya bandari ya kwa pamoja na kutatua tatizo la foleni ya malori yanayosafirisha mizigo katika barabara zinazoingia bandarini ili kupunguza tatizo lililopo na kwamba maoni na ushauri uliotolewa unafanyiwa kazi.

Mwenyekiti wa Chama Cha Wakala wa Meli Tanzania (TASAA) Daniel Mallongo, Katibu wa Chama Cha Mawakala wa Forodha (TAFF) Elinutu Mallamila na Mdau mwingine Rukia Saleh pamoja na kupongeza mikakati mbalimbali ya uboreshaji wa bandari wameomba kushughulikia haraka changamoto hizo ili kuongeza ufanisi na hivyo kuendelea kuaminiwa na watu wengi wakiwemo wa kutoka Nchi nyingine.

Wadau waliokutana katika Kikao hicho ni pamoja na Chama Cha wapokeaji na wasafirishaji wa mizigo Tanzania (TAFFA), Wadau wa Meli na Mizigo (SA/CFA), Chama Cha Mawakala wa Meli Tanzania (TASAA), Baraza la Wasafirishaji Meli Tanzania (TSC) na wengine.

Habari Zifananazo

Back to top button