TAWTO wakarabati jengo la polisi dawati la jinsia
CHAMA cha Wanawake Mawakala wa Utalii Tanzania (TAWTO) wamekarabati jengo la polisi la Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Arusha kwa kuwekwa samani za vitu mbalimbali ikiwemo michoro mbalimbali inayovutia watoto wanaofanyiwa ukatili kueleza zaidi changamoto wanazokumbana nazo kwenye jamii.
Akikabidhi jengo hilo jijini Arusha, Mwenyekiti wa TAWTO, Elizabeth Ayo amesema chama hicho kimeona umuhimu wa kukarabati jengo la dawati hilo ili kusaidia watoa huduma ambao ni jeshi la polisi kuhakikisha wanatoa huduma vizuri kwa wateja ambao ni watoto
Amesema chama hicho kimeamua kukarabati jengo hilo na kuweka samani na michoro ya eneo husika ili kuwezesha wahanga wa ukatili kutoa dukuduku zao eneo husika lenye mazingira mazuri sanjari na utoaji haki kwa wahanga wa ukatili.
“kidogo tulichojaliwa kama chama tunakitoa kwa ajili ya kushika mkono serikali ili jamii iweze kupata haki sanjari na mazingira rafiki kwa wahusika”
Akisoma taarifa fupi ,Mkaguzi Msaidizi wa Polisi ambaye ni Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Arusha,Ursula Mosha amesema dawati hilo na watoto ni lenye kusaidia jamii kuhusu kupinga unyanyasaji wa kijinsia wanaofanyiwa wanawake , watoto na wanaume ambapo awali dawati hilo lilianzishwa mwaka 2010 kwa kuhudumia jamii na kushauri dhidi ya u dawati kutoa changamoto zao za ukatili.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella alikishukuru chama hicho kwa kujitolea kusadia jamii kwani wanafanya mambo makubwa katika kuhakikisha uchumi wa nchi unakua kupitia sekta ya utalii.
“Hiki mlichofanya mungu atawalipa sababu kunawatu wanataabika na unyanyasaji ikiwemo ukatili wa watoto,wanawake na kinababa sasa ukarabati huu utatoa ari zaidi katika kutafuta suluhu ya changamoto za ukatili ikiwemo kulinda haki za watoto na kinamama “