TCAA yakabidhi msaada Polisi Mtwara

MAMALAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imetoa vifaa vya ofisi kwa jeshi la polisi kituo cha Uwanja wa Ndege wa Mtwara kama sehemu ya mamlaka hiyo kurudisha faida jamii.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni  tano vimekabidhiwa leo na Mkurungezi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari katika Uwanja wa Ndege mkoani Mtwara.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi, Johari amesema vifaa hivyo vinatokana na ahadi iloyotolewa na Bodi ya Wakurungezi wa TCAA ilipotembelea Uwanja wa Ndege wa Mtwara Julai 2022.

“Baada ya kujionea mazingira husika Bodi ya TCAA ilitoa ahadi ya kutoa vifaa vya ofisi ikiwemo kompyuta ya mezani, printa,” amesema na kuongeza kuwa vifaa vingine ni viti vya kukalia vya ofisi, viti vya kusubiria wageni, meza ya kuwekea kompyuta pamoja na kabati.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Mtwara Isaac Mushi ameshukuru mamlaka hiyo kwa kuwapa vifaa hivyo, huku akisema kwamba vitasaidia Jeshi la polisi kuboresha utoaji wa huduma zao na kuleta ufanisi mkubwa katika utendaji wao kituo cha Polisi Uwanja wa Ndege Mtwara.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x