TCAA yavunja ukimya taarifa za ndege iliyokodiwa na CHADEMA

DAR ES SALAAM: MAMLAKA ya usafiri wa anga Tanzania TCAA imetoa ufafanuzi wa habari iliyosambaa kuhusu kibali cha ndege iliyokodiwa na Chadema .
Ufafanuzi huo umetolewa kupitia mitandao yao ya kijamii ya mamlaka hiyo Oktoba 31.

2023 na kueleza kuwa

 
“Hivi karibuni vyombo kadhaa vya habari vimechapisha habari kuhusu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania kutotoa kibali kwa ndege aina ya helikopta iliyokodiwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mamlaka imesikitishwa na habari hii iliyoegemea upande mmoja hivyo kupotosha Umma na watanzania .
 
” Mamlaka inapenda kufafanua kwamba, siku za hivi karibuni hakuna Chama chochote cha kisiasa kilichoomba kibali cha kuingiza ndege nchini hata hivyo tarehe 20, Oktoba 2023 mamlaka ilipokea ombi kutoka kwa wakala wa vibali vya ndege kwa ajili ya kuainisha maeneo ambayo viongozi wa CHADEMA watakuwa wakiruka na kutua katika maeneo yasiyo rasmi lengo la kufanya mikutano ya hadhara .
 
Aidha hakuna nyaraka zozote zilizowasilishwa kwenye mamlaka kwa ajili ya maombi ya kuingiza ndege nchini kwa mujibu wa sheria.
 
“Wakala huyo alishauriwa kuwasilisha ombi la kibali cha kuingiza ndege nchini kupitia mfumo rasmi ili wataalamu wetu waweze kufanya ukaguzi wa nyaraka na pia kujiridhisha na hali ya maeneo ambayo ndege hiyo ilitarajiwa kutua na kuruka kwa mujibu wa sheria ya usafiri wa Anga, sura ya 80 pamoja na kanuni zake kupitia AIC 07/22 ((White 161 07 OCT,doc .No.TCAA /FRM/ANS/AIM/-30.
 
Wakala huyo hajawahi kurudi kwetu tena maombi rasmi kama aliyoelekezwa mpaka siku ya leo tunapotoa ufafanuzi huu kwa Umma”Kimeandika chanzo hicho mitandaoni
 
Aidha mamlaka hiyo imeongezea kwa kuandika haina sababu ya kukataa kibali cha ndege ikiwa ombi na nyaraka zinakidhi vigezo.

Habari Zifananazo

Back to top button