TCB yaanza mwaka vizuri

DAR ES SALAAM :BENKI ya Biashara Tanzania (TCB),  imesema itaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kuwekeza zaidi katika mifumo ya kidigitali hali itakayosaidia kuwafikia wananchi wengi na kuchangia ukuaji wa uchumi jumuishi nchini

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Adam Mihayo kuelezea changamoto, mikakati na mafanikio ya benki hiyo.

Amebainisha kuwa robo ya kwanza ya mwaka 2024, TCB imepata faida kabla ya kodi ya takribani Sh bilioni 13.6, ikilinganishwa na Sh bilioni 3.0 iliyopatikana kipindi kama hicho mwaka 2023, huku wastani wa mikopo chechefu ikiwa ni asilimia 3.97 ambayo ni chini ya wastani uliowekwa na Benki Kuu (BoT)

 

Habari Zifananazo

Back to top button