TCAA kuteta na wadau sekta ya anga

DAR ES SALAAM: MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) inatarajia kukutana na wadau wa sekta ya anga ili kujadili mafanikio na changamoto wanazokumbana nazo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzisha kwa Mamlaka hiyo.

Mjadala huo unatarajiwa kufanyika OKtoba 30, Mwaka huu katika ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) uliopo Dar es salaam ambapo mgeni rasmi anatarijiwa kuwa Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo, Mellania Kasese alisema hayo mkoani hapo wakati akizungumza na waandishi wa habari.

“Katika mjadala huu wadau wataongea na kujadili mambo ambayo yanayohusu usafiri wa anga kuanzia mafanikio changamoto na nini kifanyike ili kuendelea kuboresha huduma zinazotolewa na TCAA,” alisema Kasese.

Pia alisema katika muendelezo wa maadhimisho hayo OKtoba 29, Mwaka huu wanatarajia kuwa na mbio za mashindano ya ridhaa “Fun Run” zitakazoanzia Mlimani City na kuishia hapo zikiwa na lengo la kuhamasisha upandaji na utunzaji wa miti katika Mikoa yenye ukame.

“Tunafahamu kuwa uhuaribufu wa hali ya Mazingira huko angani ndio maana tumeona kitu ambacho tunaweza tukafanya ni kutumia mbio hizi kama sehemu ya kuunga mkono jamii zinazojuhusisha na utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti kwenye Mikoa kame kama Dodoma ambapo Agosti tulipanda miti kwenye shule ya msingi Chandege na kuna vikundi vya upandaji miti cha mlima Kilimanjaro,” alisema.

Kasese aliongeza kuwa “Maandalizi ya mbio hizi yamekamilika na tunatarajia kuwa na wakimbiaji wasiopungua 400 na mgeni rasmi anatarajia kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila,” aliongeza.

Katibu wa Chama Cha Riadha Mkoa wa Dar es salaam, Samweli Mwera alisema wameshirikiana na TCAA katika maandalizi yote ili kuhakikisha mbio hizo zinafanyika na katika hali ya usalama na kufukisha ujumbe kwa jamii kama ilivyokusudiwa.

“Njia watakazokimbilia za mita tano na kumi tumehakisha zimezipima na zipo katika hali ya salama,” alisema Mweri.

Alisema michezo ni sehemu ambayo inafikisha ujumbe kwa haraka kwa watu wote hivyo wanaamini mbio hizo zitafikisha ujumbe wa kupanda na kutunza miti vizuri.

Habari Zifananazo

Back to top button