RAIS wa Chemba ya Wafanyabiashara,Viwanda na Kilimo (TCCIA) Vicent Bruno amefanya ziara ya kutembelea baadhi ya miradi ya kimkakati iliyopo mkoani Mtwara.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, rais huyo wa TCCIA amesema lengo la ziara hiyo ni kujua maendeleo, kuona ushirikiano uliyopo kati ya Chemba na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali ya Mkoa.
Miongoni mwa miradi aliyotembelea ikiwemo kiwanda cha kubangua korosho cha COSONUT, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na kiwanda cha kuzalisha saruji cha Dangote.
Amesema amejionea fursa nyingi zilizopo mkoani humo ikiwemo bandari huku akiahidi kuitangaza bandari nje ya nchi ili wawekezaji watakaofika mtwara wapitishie bidhaa zao.
Kaimu Meneja TPA Mkoa wa Mtwara, James Ngw’andu amesema kwasasa changamoto ya vumbi la makaa ya mawe lililokuwa likiwaathiri wananchi waishio pembenzoni mwa bandari imepungua tofauti na mwanzo wakati biashara hiyo ilikuwa mpya.
Hata hivyo uongozi wa tpa katika kutatua kabisa changamoto hiyo teyari wameshatenga eneo kwa ajili ya kujenga bandari ya kubeba mizigo michafu lililopo kisiwa mgao halmshauri ya wilaya ya Mtwara mkoani humo.
Amesema kwa sasa bandari hiyo ina uwezo wa kuhudumia zaidi ya tani milioni 1 kwa mwaka kufuatia uwekezaji mkubwa uliyofanywa na serikali bandarini hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas amesema kutokana na kufungwa kwa shughuri za mpaka wa kusini kwa mwaka 2023 kulipelekea changamoto ya mdororo wa kibiashara ndani ya mkoa na wilaya kwa ujumla.
“Tayari tulishafanya mazungumzo na tra na vyombo vingine vinavyohusika kwenye mnyororo wa thamani wa kibiashara ili kulegeza masharti bila kuathiri uchumi wa taifa na mkoa”.
amesema Abbas