TCCIA yasuka mikakati mipya biashara mikoani

DAR ES SALAAM; Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA),Oscar Kisanga, amesema atasuka mikakati mipya kuanzisha programu za kuwajengea uwezo na kuwatembelea wafanyabishara na wakulima katika maeneno mbalimbali nchini.

Kisanga amesema hayo leo jijini Dar es Salaam baada ya kuchaguliwa na Halmashauri Kuu ya TCCIA kuwa mtendaji mpya.

“Nitashirikiana na wafanyabishara ili kusikiliza hoja zao nitakuja na mikakati ya muda mfupi na mrefu, ambayo itatoa majibu ya wapi tupo na wapi tunakwenda na kwa kuangalia huko tutajua changamoto na jinsi ya kutatua na kufahamu matarajio ya wanachemba ni yepi na wapi wanakwenda,”ameeleza.

Amesema kupitia programu hizo atatembea mikoani na wilayani, ili kuzungumza na wafanyabishara na wakulima kujua wanakwama wapi.

“Nitashirikiana na wafanyakazi wenzangu na wafanyabishara wote kuanzia wilayani, mikoani na Taifa na vilevile nitashirikiana na wadau na serikali kwa nafasi hii naomba ushirikiano wao nitafanya kazi kwa kujitahidi, ili kuleta matokeo chanya katika chemba hii ya wafanyabishara kwa upande wa viwanda, kilimo pamoja na biashara,”amesisitiza Kisanga.

Amefafanua kuwa atahakikisha TCCIA inarudi na kufanya kazi kwa weledi ili kujibu matakwa ya wafanyabishara.

Kwa upande wake Rais wa TCCIA, Vicent Minja amesema walianza mchakato wa kumpata mtendaji huyo tangu mwaka jana ambapo halmashauri kuu ya chemba imemthibisha kwa kura zote.

“Tumekuwa na pengo kwa zaidi ya miaka mitano walikuwa wanakaimu na hii ilikuwa inatusumbua sana tukaona tulipe mkazo na wajumbe wote 31 wameshiriki,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button