TCRA kudili na matapeli mitandaoni

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuna haja ya kuwadhibiti wanaotumia mitandao vibaya kwa kufanya matukio ya utapeli kuiba taarifa binafsi za watumiaji wengine kwa lengo la kujinufaisha wenye na hata kuleta matatizo kwa wengine.

Aidha imesema ni muhimu elimu kuhusu usalama wa mtandao kutolewa kwa kila nyanja ili kudhibiti wahalifu hao na pengine kuwatia katika kundi hilo na kuingia kwenye kuelimisha kwa usalama wa mtandao.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA,Jabir Bakari amesema hayo Leo Dar es Salaam wakati akizungumza na makundi mbalimbali ya wajasiriamali ikiwa ni kuelekea siku ya usalama wa mtandao duniani.kila jumanne ya pili ya februari kila mwaka,Dunia huadhimisha siku ya usalama wa mitandao.

Advertisement

Kuhusu uhalifu mtandaoni amesema pamoja na faida za mitandao bado ipo haja Kwa wahalifu wa mtandao kudhibitiwa na kupewa elimu na kutoka kwenye kundi hilo la uhalifu na kuwaelimisha wengine kuhusu usalama wa mitandao.

” Kupitia mitandao unaweza kuongeza kipato na pengine kuwa na ubunifu ama ajira jambo linaloweza kubadilisha maisha ,” amesema Bakari na kuongeza kuwa teknolojia ya kidigiti inaongeza wigo wa Mawasiliano.

Ametolea mfano kuwa dereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda anayetumia Tehama anafikiwa na fursa nyingi kuliko asiyekuwa na nafasi hiyo hivyo hivyo na kwa mamalishe wanaotumia fursa kama hizo.

Amesema matumizi salama ya mtandaoni ni jukumu la kila mmoja ili mtandao uwe sehemu salama, inatakiwa kuwe na kizazi chenye kujua Tehama Ili kukuza jamii iliyo kamilifu kushiriki uchumi wa kidigitali.

Amesema katika siku za karibuni Kuna maendeleo makubwa ya Mawasiliano ndani na nje ya nchi ambapo hadi kufikia Desemba mwaka jana 2023 kwa Tanzania watumiaji wa mtandao wamefikia milioni 35.8.

Amesema idadi ya simu janja imefikia milioni 19.

8 jambo linaloonesha kuwa na mabadiliko makubwa na lakini za simu ni milioni 70 huku kati ya hizi lakini milioni 51 hazipo kwenye mitandao ya intanent.

“Dira ni kuwa na jamii iliyowezeshwa kimtandao kwa huduma za mawasiliano zipatikane kila wakati,” alisema na kuongeza kuwa katika zama za mwendo wa kidigiti ni muhimu Sana kuwa na wajibu wa elimu endelevu ya usalama wa mtandao,” amesema.

Bakari amesema katika kukuza mtamdao lengo ni kuwezesha Wahandisi nchini kuwa na uwezo wa kutengeneza mifumo ya mitandao badala ya kuwa watumiaji pekee,kwamba matumizi ya Tehama yalete tija nchini.

Mmoja wa mshiriki katika mafunzo hayo, Dk Macca Abdalla amesema kuwa wafanyabiashara ndogondogo waunganishwe pamoja kupitia dirisha Moja ili kuwaibua wanawake wa chini waweze kukuza viparo vyao na kuendesha Biashara zao Kwa nyanja mbalimbali ikiwemo mitandao

Kuhusu mtandao amesema imewasaidia kwa kukuza bidhaa zao na pengine kutumiwa au kutuma fedha badala ya kufuatilia mmoja mmoja.