MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewafungulia milango vijana wabunifu katika Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa kuwapa uwezeshaji uliokuwa unakwamisha ubunifu miaka yote nchini.
Akizungumza leo Novemba 14, Mkurugenzi wa TCRA, Dk Jabir Bakari amesema TCRA kwa ushirikiano na taasisi nyingine imeweka mazingira rafiki kwa vijana wabunifu wa TEHAMA kutengeneza fursa za kukuza ubunifu na hatimaye kuzaa.
amesema Rasilimali za mawasiliano zinazotolewa na TCRA kwa ajili ya vijana wabunifu kufanya majaribio ni pamoja na misimbo ya USSD, yaani rasilimali-namba.
“Hizi ni namba maalum zinazotumika kumpa mbunifu fursa ya kusambaza teknolojia aliyoibuni ndani na nje ya nchi. Pia TCRA kwa sasa wanatoa kikoa (domain) cha dot tz (.tz) na masafa ya mawasiliano.”Amesema
Aidha, amesema TCRA imeweka utaratibu wa kusaidia vijana kwa kuweka utaratibu wa kutoa rasilimali hizo kwa muda wa miezi mitatu.