TCRA yatoa tahadhari kwa watumiaji huduma za kifedha

ARUSHA; Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa rai Kwa watumiaji wa huduma za kifedha katika mitandao ya simu kujiridhisha kwenye vyanzo husika juu ya taarifa wanazopokea kabla ya kutuma fedha zao.

Akiongea katika viwanja vya Sheikh Amir Abed jijini Arusha katika maonesho ya tatu ya wiki za huduma za kifedha kitaifa 2023, Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa TCRA, Semu Mwakyanjala amesema kuwa ni vema wananchi wakapata maelekezo ya mtandao husika ili kuepuka kutapeliwa.

“TCRA inashauri watumiaji wa huduma za simu za kiganjani kuhakikisha taarifa wanazopokea za kuwataka kutuma fedha kujiridhisha kutoka kwenye kampuni husika, kabla ya kutuma fedha ili kujiepusha na matapeli,”amesema

Aidha aliwatoa hofu watumiaji wa huduma za kifedha kuhusu kuibiwa fedha zao na matapeli wa mitandao, kwaninserikali imeweka mifumo imara ya udhibiti hilo.

“Natoa onyo kwa matapeli wanaojipanga kuibia watu kupitia mitandao kuacha kwani hawatakua salama kwani vyombo vya usalama ikiwemo jeshi la polisi vipo macho kudhibiti watu hawa,”.

Kwa mujibu wa Mwakyanjala amesema Tanzania ni nchi ya pili kwa utoaji huduma bora za kifedha kati ya nchi 55 Afrika.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
kujipiga NONDO NA KUJICHUNA NGOZI
kujipiga NONDO NA KUJICHUNA NGOZI
16 days ago

Ajiuwa kwa kujipiga NONDO NA KUJICHUNA NGOZI na kumpelekea bosi wake – kwa sababu ya mapenzi na kutakiwa kujua maisha ya watu wengi zaidi ya million 7

Capture.JPG
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x