JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limeeleza ya kwamba nchi zilizoendelea, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imekuwa chanzo kikubwa cha kukuza mitaji ya watu.
Hivyo limepongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF),kwa hatua yake ya uwekezaji wa ubia uliofanywa na umeonesha ukomavu wa mfuko huo katika kukuza uchumi wa watu.
Mwenyekiti TEF, Deodatus Balile amesema hayo Machi 31, 2023 wakati wa ziara ya wahariri wa kutoka vyombo mbalimbali vya habari katika Kiwanda na Machinjio ya kisasa ya Nguru Hills , yaliyopo katika wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.
Wahariri walioshiriki mkutano wa 12 wa Jukwaa la Wahariri Tanzania kuanzia Machi 28, hadi Aprili Mosi mwaka huu (2023) Mjini Morogoro.
“Niwaombe PSSSF wahakikishe mradi huu wanaulinda na miradi mingine, si vyema sana baada ya miaka kadhaa mbele ukija tena tuambiwe kilikuwepo kiwanda kisa wafanyakazi hawakutimiza wajibu wao vizuri”amesema Balile
Naye Meneja mkuu wa Kiwanda na Machinjio ya kisasa ya Nguru Hills , Eric Cormack amesema mradi huo unaowezo wa kuchinja ng’ombe 100 na mbuzi 1,500 kwa siku.
Amesema soko la nyama inayozalishwa kwenye mashinchinjo hayo imepata soko la nje ya nchi kwa asilimia 80 zikiwemo za mashariki ya kati hasa ya Oman ,na asilimia 20 kwa ajili ya soko la ndani .
“ Tumekuwa tukisafirisha zaidi nyama kwenda nchini Qatar hasa kipindi cha kombe la dunia na tunaendelea hadi kwa nyama kama mbuzi na kondoo na soko linendelea kupanuka kwenye nchi za Kiarabu” amesema Cormack
Amesema mahitaji ya nyama katika nchi hizo bado ni makubwa huku akitolea mfano mahitaji kwa nchi ya Saudi Arabia pekee mahitaji yao kwa mwaka ni tani 700,000.
Cormack amesema kwa nchi za kiarabu mahitaji ya nyama yataongezeka zaidi kufikia mwaka 2026 kwa tani milioni 3, 100,000
Amesema mradi una miundombinu muhimu ikiwemo eneo la malisho lenye ukubwa hekta 2, 328, kutunza Ng’ombe 10,000 na Mbuzi 15,000 kwa wakati mmoja, na visima vitano yenye uwezo wa kuzalisha lita 20,000 kwa saa.
Cormack amesema usafirishaji wa nyama utaongezeka katika kipindi kifupi kijacho baada ya kupaatikana kibali cha ISO kwa bidhaa za kiwanda hicho kuweza kutambulika kimataifa, na hiyo itakuwa rahisi kuuza bidhaa zao kwenye mataifa mbalimbali Duniani na hasa Saudi Arabia.