‘Tehama sasa ni ya kujenga uchumi jumuishi’

DSM; Mkurugenzi wa Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), Dk. Nkudwe Mwasaga amesema Tehama ya sasa hivi ni ya kujenga uchumi wa kidijitali, ambao ni jumuishi kwa watu wa aina zote na rika zote pamoja na wenye mahitaji maalum.

Amesema hayo leo Oktoba 17 kwenye kongamano la saba la Tehama Tanzania lililoanza jana na litafanyika kwa mda wa siku tano jijini Dar es salaam.

Mwasanga amesema kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ha Habari, wametoa ufadhili Kwa vijana 130 kutoka mikoa mbalimbali nchini kuja kushiriki kongamano hilo, ili kuwajengea kujiamini na wakawe wabunifu mahiri kwenye utendaji kazi.

Naye Mkuu wa huduma za kiufundi katika Tume ya Tehama, Mhandisi Jason Ndagunzi amesema mkutano wa leo umekutanisha vijana na kuwapa fursa ya kutoa maoni, ushauri na michango walio nayo kwenye nyanja ya Tehama kwa lengo la kunufaisha Taifa.

Mkutano huo unaendelea kesho na kukutanisha kampuni na taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi na kujadili maendeleo na changamoto za Tehama, ili kupata suluhisho bora.

Habari Zifananazo

Back to top button