Teknolojia ya vifuu katika uchenjuaji madini inavyookoa gharama, mazingira  

Ubunifu na ukuaji wa matumizi ya teknolojia ni hatua  muhimu katika jamii iliyolenga kujikwamua au kutatua changamoto lukuki zinazoikabili.
Kwa vijana, ubunifu ni mbinu nyingine ya ya kujiajiri hasa ikizingatiwa kuwa ukosefu wa ajira umekuwa ukiliathiri kundi hilo kwa miaka ya hivi karibuni.
Katika kutumiza azma hiyo kwa vijana kwa kusaidia kazi za  kibunifu, serikali,  kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imekuwa ikiwawezesha wabunifu mbalimbali kwa kuwapa fedha ili waweze kutumia kazi zao kuleta maendeleo katika jamii.
Kupitia programu hiyo, kifuu cha nazi kinapata thamani kutoka kuwa uchafu au nyenzo ya kuwashia moto na kuwa malighafi ya thamani kwa kuiangiza kipato.
Ukiachana na faida za mafuta ya nazi ambayo wengi hutumika kama dawa ya magonjwa ya ngozi, vifuu sasa vinaelezwa kuwa na faida kubwa pale vinapotunika  kutengeneza vitu vya sanaa kama vyombo vya kitamaduni pamoja na urembo.
Vile vile kutengenezwa kuwa vijiko au nyuma, kupandia maua, mwonekano wake mzuri unaweza kutumia kamba kuning’iniza na kutumia kupanda maua na kupendezesha nyumba yako.
Pia hutumika kutengeneza pochi nzuri yenye mpangilio mzuri na vihifadhio. Hii ni kwa sababu ikiwa vifuu vya nazi vitasafishwa vizuri na kuwekwa kwa mpangilio mzuri huweza kutumia kupangilia na kuhifadhi vitu kama hereni, sabuni, vipodozi, pesa na na vifaa vidogo kama pini ambavyo ni rahisi kupotea. .
Kifuu cha nazi kinaweza kutumika kutengeneza mapambo kama hereni, bangili, vifungo na mikufu.
Uchenjuaji wa madini
 
Ubunifu mkubwa umefanyika hapa nchini wa kutengenza kaboni (Carbon) kwa ajili ya kuchenjulia madini, kusafisha maji kwa kutumia vifuu vya nazi.
Mtafiti na mbunifu wa teknolojia ya kutengeneza Carbone, Tiberius Mario anasema baada ya kufanya tafiti alikuja kugundua kuwa vifuu vya nazi vinaweza kutengeneza coboni ambayo ni salama kwa mazingira katika shughuli za madini.
Anasema ubunifu huo alioufanya una nafasi kubwa ya kudhibiti uchafunzi wa mazingira. “Tunatengeneza ‘Activated Carbon’ kutoka katika vifuu vya nazi.”
Kwa mujibu wa mtaalam huyo,  kupitia vichembechembe  vidogovidogo vya kaboni, wanatengenezea matundu ndani vinakuwa na corosite ndani hivyo vitundu vinatumika kukamatisha dhahabu.
“Nimeegemea sana kwenye upande wa dhahabu na maji machafu ninabadilisha kifuu cha nazi kwenda kwenye Carbon ambayo kwenye migodi yote Tanzania huwezi kupata dhahabu bila ya kuwa na Carbon ambapo udongo baada ya kuchujwa lazima upitishwe kwenye carbon ndipo dhahabu zitoke kwenye udongo,” anasisitiza.
Anasema hapa nchini hakuna kiwanda cha kutengeneza Carbon kwa asilimia 100 zinatoka nje ya nchi wakati mikoa ya Pwani na Kusini kuna nazi nyingi zaidi ya tani 350,000 kwa mwaka ambapo hutoa vifuu vingi.
Anabainisha kuwa ameona abadilishe na kuwa kitu chenye thamani kwa kutengeneza carbon.
“Nilifanya utafiti wa kuzalisha kidogo sasa nazalisha za wastani na nilishapeleka kwenye baadhi ya migodi pia katika viwanda vya maji inatumika kusafisha maji kwa kupinguza clorine katika maji ili yaweze kutumika na kuondoa harufu.
Mario anasema katika orodha ya nchi zinazozalisha zao la nazi kwa wingi duniani, India inaongoza ikifuatiwa na Indonesia. Tanzania inashika nafasi ya
 16 ikiwa na uwezo wa kuzalisha tani 382,164 kwa mwaka, akiashiria kuwa kuna uwezekano wa kuzalisha vifuu vingi zaidi.
“Endapo vifuu vya havitahifadhiwa barabara  vinaweza kusababisha magonjwa. Hii ni kwa sababu ya kugeuka mazalia ya mbu endapo vikinyeshewa na mvua,” anasema na kuongeza: “Mbali na kuenea kwa malaria kupitia mbu, vifuu huhifadhi uchafu unaoweza kusababisha kipindupindu.”
Unafuu wa vifuu
 
Anasema Tanzania inaagiza zaidi ya tani 1,500 za kaboni, hivyo hupoteza takribani ni dola milioni 6.7 Kwa mwaka.
“Vifuu hiyo ninayotengeneza vinaenda kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini kwani vina gharama nafuu. Kuna wakati kaboni inayoagizwa inaadimika kama wakati wa Corona,” anaeleza Mario.
Aidha anafafanua kuwa kaboni hiyo imeweza kupimwa katika maabara na utendaji wake ni asilimia 98 katika madini na maji asilimia 98.
“Nilipeleka Mbeya, Shelui na Stamico na nilichukua sampuli nikapeleka Tme ya Madini, matokeo yalitoka mazuri imekamata dhahabu kwa kiwango kikubwa na pia ninaweza kurudisha tena kwenye kwenye mfumo kaboni ambayo inatumika kwani ikitumika haitakiwi kutupwa ila zinahifadhiwa hivyo ili kuondoa mrundikano,” mbunifu anaeleza.
Changamoto
 
Mario anasema changamoto zinazomkabili ni mtaji wa kufanya uzalijishaji ambapo sasa anazalisha kilo 100 huku mahitaji yakiwa no makubwa.
Pia anasema chanzo cha joto anayotumia ni makaa ya mawe na kuni ambapo kitaalamu anahitaji joto zaidi ya 300,000 lakini kuni inanipa joto la 4000 kwa kilo moja ili kupata 300000 ninatumia kuni nyingi na muda ni mrefu.
“Nikipata ‘diesel burn’ joto lake ni kubwa ikilinganishwa na kuni na kifaa kinachotumika tutengeneza na kutoa bidhaa ninayotoa mimi ifike hata asilimia 90 sasa ni asilimi 50 nikiwezeshwa ninaweza kuchukua vifuu vyote na kutengeneza Kaboni hatutaagiza nje nahitaji Sh milioni 36,” anaeleza.
Kwa mujibu wa bei ya soko, mfuko mmoja wa kilo 25 unauzwa Sh 250,000 hadi Sh 400,000. Wakati mwingine bei inategemea bidhaa hiyo inatoka wapi. Mathalan Kwa kiwango Cha ujazo kama huo, nchini China wanauza Sh 250,000 na Sh 280,000 na Amerika ni Sh 400,000 na kwa lakini rejareja kilo moja 20,000 hadi 25,000.
Mtafiti na mbunifu wa teknolojia ya kutengeneza Carbone, Tiberius Mario akieleza namna anavyobadilisha vifuu vya nazi kuwa kaboni ya kuchenjulia madini
“Ni kitu cha gharama inaweza kuhitaji hata kilo 500 lakini uwezo wangu ni mdogo nikipata mtaji nitafanya vizuri, sina nazi peke yake hata mchikichi naweza kutumia,” anasisitiza Mario.
Anasema Tanzania ina uwezo wa kuokoa dola za kimarekani mulioni 6 zinazotumika kuagiza kaboni nje ya nchi.
Mikakati wa TARI
 
Mratibu wa Uhaulishaji Teknolojia na Mahusiano kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) katika kituo cha Mikocheni jijini Dar es Salaam, Vidah Mahava anasema bado kuna uhitaji mkubwa wa zao la nazi ambapo kwani hata wadau wengine wanaotumia nazi kama malighafi wanalazimika kuagiza nje ya nchi.
Mtafiti na mbunifu wa Teknolojia ya kutengeneza Carbone ,Tiberius Mario akiwaonesha waandishi wa habari vifaa anavyotumia kutengeneza carbon kwaajili ya kuchenjulia madini.

 

Mahava anasema mara nyingi wamekuwa wakiwashauri wakulima wa zao hilo kulima kwa kufuata kanuni bora za kilimo na kutumia miche yao ambayo imefanyiwa utafiti na kuipatia huduma bora ili iweze kuzaa zaidi.
Anasema kwa sasa nazi ina mahitaji mengi na zinahitajika sana kutokana na matumizi yake.
“Naomba niwaambie kwamba hata nazi mnazoziona watu wanazozipikia bado mahitaji ni makubwa na zile zinazotumika viwandani nyingine zinaagizwa kutoka nje ya nchi,” anaeleza.
AnasemaTARI-Mikocheni ni moja kati ya vituo 17 vinavyofanya utafiti wa kilimo na kuendeleza zao la minazi na kusimamia masuala yote ya bayoteknolojia.
Anafafanua kuwa minazi inaanza kuzaa kuanzia miaka mitano hadi saba na lakini hapa katikati iliwahi kuletwa minazi inayoanza kuzaa miaka mitatu lakini bado ilionekana haifanyi vizuri na  inaonekana ikizaa baada ya muda mfupi inakufa kutokana na magonjwa na haikuweza kustahimili hali ya hewa.
“Lakini minazi ambayo tumefanyia utafiti na ambayo tunasambaza sasa ni hii minazi ya asili inayoitwa East African Tall ambayo inaanza kuzaa baada ya miaka mitano hadi saba na inaweza kuzaa hadi nazi 70 na kuendelea lakini pia tunaendelea kufanyia utafiti zaidi ili iweze kuzaa nazi nyingi zaidi zinazofikia 100 na kuendelea,” alibainisha.
Aidha anabainisha kuwa idadi kubwa ya minazi mingi iliyopo ni ile ambayo wamepanda miaka mingi iliyopita na mara nyingi TARI imekuwa ikishauri   wadau kwamba waanze kupanda minazi mipya na ile iliyopo waitunze kwa kufuata kanuni bora za kilimo.

Habari Zifananazo

Back to top button