Teknolojia yabadilisha mifumo ya kijamii

MABADILIKO ya kidijitali na teknolojia yamebadilisha mifumo katika jamii kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na kuleta mabadiliko zaidi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society ( FCS), Francis Kiwanga alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari ikiwa ni maandalizi ya Wiki ya Asasi za Kiraia ( Azaki), itakayofanyika Oktoba 23 mpaka 27 jijini Arusha.

Kiwanga alisema kama kauli mbiu ya wiki hiyo inavyosema, ‘ Teknolojia na Jamii’ majadiliano juu ya makutano ya teknolojia na jamii ni muhimu ili kuelewa mabadiliko hayo.

Ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto zilizopo katika jamii kwa kutumia fursa zinazotolewa.

“Suala kubwa tunalozungumza sisi kama wanaazaki ni kujitathnini kwa kiasi gani tunaweza kutumia teknolojia katika miradi na kazi zetu?ni maeneo gani ambayo tumejifunza au ni maeneo gani yana changamoto,? alihoji.

Alitaja malengo ya wiki hiyo kuwa ni ujumuishwaji wa teknolojia kwenye kazi za azaki, kuziwezesha na kuzipa nguvu jamii zilizotengwa, utetezi, ushirikiano na uchechemuzi wa kidijitali.

Naye Mkurugenzi Mkazi Malala Foundation, Nuria Mshau alitaja mada zitakazokuwepo kuwa ni ujumuishaji na uwezeshaji wakidijitali, matumizi ya takwimu kuleta manufaa kwa jamii,

Vile vile teknolojia na utetezi wa kijamii pamoja na elimu na mafunzo ya dijitali nchini Tanzania.

Naye Doreen Dominic Kutoka benki ya Stanbic alisema ushiriki wao katika wiki hiyo unachochewa na ushirikiano na ubunifu.

“Tunaelewa uwezo wa teknolojia katika kuendeleza maendeleo ya kijamii na kutatua changamoto muhimu zinazokabiliwa na nchi. Uwepo wetu kwenye tukio hili unalenga kuunganisha mashiirika na wateja,” alisema.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x