Teknolojia yongeza ufaulu

UTUMIAJI wa teknolojia katika elimu umewezesha kuinua kiwango cha ufaulu hususan katika maeneo ambayo hayana maabara ama walimu wa kutosha.

Hili limedhihirika wakati Mkurugenzi wa mikakati kutoka Kampuni ya Smart Darasa mkoani Dar es Salaam, Kusiluka Aginiwe alipoeleza jinsi ambavyo fedha za serikali kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), zilivyochangia kuongeza ufaulu kwa kutumia jukwaa lao la elimu kwa mtandao.

Aginiwe alisema kupitia jukwao lao la smart darasa wamejikita kwa wanafunzi na walimu kujifunza masomo ya sayansi kwa vitendo kwa kutumia vifaa vya kidijitali.

“Smart darasa pia tunamsaidia mwalimu kuweza kuandaa vifaa vya kufundishia kwa vitendo kwa maana mwalimu hata kama hawana maabara ndani ya shule anaweza akatumia jukwaa la smart darasa kuonyesha majaribio Fulani yanafanyaje kazi na vitu mbalimbali,” alisema.

Aliipongeza hatua ya serikali kwenye mageuzi ya kidijitali kwa maana imeweza kusambaza vishikwambi kwa walimu wote katika shule zote za serikali nchini, ambayo ni hatua kubwa kwa jukwaa hilo la smart darasa kwa maana kwamba mwalimu akiwa popote Tanzania ataweza kufundisha kwa vitendo akiwa darasani hata kwa kutumia kishikwambi chake.

“Mfano huu tumeweza kuupata kwa vitendo katika shule moja iliyopo Chamazi ambayo haina maabara japokuwa ina miaka zaidi ya mitatu sasa, tulienda kuwafanyia mafunzo walimu wa ile shule na sasa wanatumia smart darasa kama maabara ya kidijitali,” alisema.

Alisema katika shule hiyo japokuwa hawana maabara kupitia jukwaa hilo wameweza kufaulisha wanafunzi wa kidato cha pili sasa hivi wanaelekea kwenda hatua ya kidato cha nne.

” Katika shule ya Chamazi kuna mzazi mmoja àmbaye ni mhandisi hii tulipata kutoka kwa walimu, sisi tulienda pale kufanya mafunzo mwezi wa saba, tukapewa ushuhuda huo ulitokea mwezi wa sita, kwa kuwa shule haina maabara na mza I ni mhandisi alimtoa mtoto wake pale.

“Wale walimu wakasema hii smart darasa ingekuwepo mwezi mmoja kabla, tunatumai yule mzazi angemwacha myoto wake,” alisema.

Alisema serikali kupitia costech imewapa ufadhili wa zaidi y ash milioni 70 kwenye ubunifu huo wa kutumia teknolojia ya kusoma kwa njia ya kidijitali ambayo imetoa matokeo chanya mpaka sasa.

Alisema japokuwa hawajajitangaza lakini wamefanikisha kupata watumiaji wa simu za android zaidi ya 2000, website zaidi ya 10,000, pia ki nchi nan chi watumiwa na Kenya, Nigeria, India na Marekani, kwa hapa Tanzania bado hawajakamilisha mfumo unaoonyesha mikoa inayotumia teknolojia hiyo kwa wingi.

Naye Mwalimu wa Nidhamu na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), wa Shule ya Sekondari Chamazi, alisema shule hiyo ina miaka mitatu lakini haina maabara, hivto teknolojia hiyo ya kufundishia kwao imekuwa ni mkombozi.

Alisema wanafunzi sasa wanafurahia masomo ya sayansi na kuyapenda.

Kwa upande wake Meneja Uhifadhi Taarifa na Machapisho Costech, Dk Philbert Luhunga alisema ziara hiyo inalenga kuonyesha jinsi fedha zinazotolewa na serikali kupitia tume hiyo zinavyotoa matokeo chanya kwa jamii.

Habari Zifananazo

Back to top button