Tembo Nickel yatabiriwa kubadilisha sekta ya madini

KAMISHNA wa Madini kutoka Tume ya Madini, Janet Lekashingo amesema mradi wa Kabanga Nickel wilayani Ngara katika Mkoa wa Kagera utaleta mabadiliko kwenye sekta ya madini nchini.

Lekashingo alisema hayo alipoutembelea mradi huo na akasema Tembo Nickel kuwa na ubia na Lifezone, BHP na Serikali ya Tanzania ni jambo linaloonyesha kampuni hiyo italeta matumaini kwa taifa.

“Mradi wa Kabanga Nickel unaoendeshawa na Kampuni ya Tembo Nickel ni mradi ambao ni muhimu sana kwetu, tunaenda kwenye madini ya kimkakati,” alisema.

Advertisement

Lekashingo pia alipongeza Tembo Nickel kufanya utafiti wa ujuzi ili kujua aina ya ujuzi ulio wilayani Ngara na kusema kuwa kufanya kazi na jamii inayozunguka mradi, ni siri ya mafanikio.

Pia alipongeza Tembo Nickel kwa kuanza programu ya kuchukua wahitimu wa vyuo vikuu kwenye fani mbalimbali na kuwapa kazi ili wajifunze kwa vitendo.

Alisema pia Tembo Nickel ni mgodi unaoanza baada ya miaka 20 tangu kuanze kuwa na migodi mikubwa nchini, hivyo alitaka uzoefu uliopatika katika kipindi hicho utumike kuhakikisha mradi huo unakuwa wa mfano.

Meneja wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi, Dk Kudra Said alisema Tembo Nickel imeshafanya utafiti wa ujuzi kwa awamu mbili katika Wilaya ya Ngara ili kupata watu wa kufanya kazi kwenye mradi.

6 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *