TEMESA yataka kulipwa madeni yao taasisi za serikali
WAKALA wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) imewakumbusha wadau mbalimbali na taasisi za serikali nchini ziweze kuwalipa deni lao la zaidi ya Sh bilioni 48 .
Hayo yamesemwa leo na Kaimu mtendaji mkuu wa Temesa mhandisi Hassan Karonda wakati wa kikao kati ya Temesa na wadau wake mkoani Mwanza.
Amesema wao kama Temesa wataendelea kuwakumbusha wadau wao kuwalipia fedha hizo. Karonda amesema wataendlea kufanya vikao mbali mbali na wadau wao ili kuweza kuendelea kuboresha huduma zao.
Amewataka wazabuni mbali mbali kuweza kuwaletea vipuri halisi vya magari. Aliweka wazi kuwa Serikali imetenga fedha bilioni 1 kwajili ya ujenzi wa karakana 12 katika maeneo tofauti tofauti nchini. Amesema wamefanikiwa kutoa mafunzo ya teknolojia mpya kwa mafundi wao 45 katika chuo cha usafirishaji(NIT) Dsm.
Naye meneja wa TEMESA mkoa wa Mwanza mhandisi Gilly Chacha amesema kwa mkoa wa Mwanza wao wanadai wadau wao zaidi ya Shilingi bilioni 1.4.
Amesema wataendelea kupokea na kufanyia kazi maombi na maoni ya wadau mbali.