Ten Hag: Bruno ataendelea kuwa nahodha

KOCHA wa Manchester United, Eric Ten Hag amesema kiungo Bruno Fernandez ataendelea kuwa nahodha wa timu hiyo pale ambapo beki Harry Maguire atakosekana uwanjani.

Ten Hag amelazimika kusema hayo kufuatia baadhi ya manguli wa soka kudai kuwa mchezaji huyo hastahili kuwa nahodha kutokana na tabia zake alizoonesha kwenye mchezo wa wikiendi iliyopita dhidi ya Liverpool.

Akizungumza leo kwenye mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kesho wa EUROPA League dhidi ya Real Betis Uwanja wa Old Trafford, Hag amesema ana furaha Bruno kuwa nahodha na kwamba kila mtu anafanya makosa.

Advertisement

“Ana kipaji nina furaha kuwa mchezaji wetu na nahodha pia”.amesema Hag.
Wiki iliyopita wachezaji wa zamani wa England, Chris Sutton na Gary Neville walimshukia kiungo huyo kuwa hafai kuwa nahodha baada ya kuonyesha tabia ambazo waliziita mbovu kwa kutowajibika na kumsukuma mwamuzi kwa ishara ya dharau.

/* */