Ten Hag: Maguire ataamua mwenyewe

SUALA la beki wa Man United, Harry Maguire kubaki klabuni hao linabaki mikononi mwake na sio tena kwa kocha Eric Ten Hag.

Muingereza huyo ,30, amecheza mechi 16 tu kati ya 38 za Ligi Kuu England msimu huu.

Pengine kauli hiyo inaweza kuwa ni sababu ya uwepo wa Lisandro Martinez na Raphael Varane ambao Ten Hag amekuwa akiwatumia kwa pamoja katika michezo mingi msimu huu.

“Hakuna atakayekuwa na furaha na hali hii, anafanya mazoezi kwa kiwango cha juu, ukapteni wake ni muhimu kwenye kikosi chetu.” Amesema Ten Hag.

Maguire amekuwa akifanya baadhi ya makosa yaliyoigharimu timu hiyo ukiwemo mchezo wa Europa dhidi ya Sevilla ambao United walifungwa mabao 3-0.

Ten Hag anaongeza: “Anapambana sana eneo la kati na Varane ambaye ni bora zaidi.”

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button