TET kushiriki kongamano la 3

Ni la Kimataifa la Huduma za Maktaba

DAR ES SALAAM: Kongamano la tatu la Kitaifa la Huduma za Maktaba,Tamasha la Vitabu na Usomaji limepangwa kuanza kesho Septemba 19 hadi 21 katika viwanja vya chuo cha Benki Kuu Mwanza (BOT) ambapo Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) itashiriki pamoja na wachapishaji mbalimbali wa vitabu nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa TET, Aneth Komba akizungumza na HabariLEO leo Septemba 19,2023 amesema kongamano hilo ni muhimu kwani vitabu ni nyezo muhimu katika suala la ufudishaji na ujifunzaji na kusema kuwa serikali itaendelea kuhamasisha jitihada za usomaji nchini .

Amesema usomaji wa vitabu unatoa ufahamu na uelewa wenye kutoa maarifa ambayo yanaishi na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kutambua umuhimu wa uchapishaji nchini .

‘’Usomaji wa vitabu ni jambo muhimu sana nchini hivyo kongamano hili ninaamini litasaidia katika kuendelea kuhamasisha usomaji wa vitabu kwa lengo la kupata maarifa ” amesema Dk Aneth

Amesema, katika kongamano hilo, TET itakua na banda ndani ya viwanja vya BOT na vitabu vyote vitapatikana hapo kwa bei nafuu.

‘Tunasisitiza usomaji wa vitabu vyote kila mwanafunzi vya kiada na ziada kwani anapojisomea vitabu tunajenga taifa lenye maarifa katika kujenga nchi yetu tunashirikiana na katika kuamsha ari mpya ya usomaji na tutaendelea kuhimiza ari ya usomaji wa vitabu, tusome vitabu vyote kwa ajili ya kupata maarifa’’ amesema Dkt.Komba

Kongamano hilo linawakutanisha wachapishaji mbalimbali na wananchi wa kawaida ambao watapata nafasi ya kusoma vitabu mbalimbali vinaoneshwa kwenye maonesho hayo.

Habari Zifananazo

Back to top button