TET, taasisi 5 zasaini mkataba

TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) imesaini makubaliano na taasisi tano zisizo za kiserikali yenye lengo la kuboresha elimu nchini katika nyanja mbalimbali.

Taasisi hizo ni pamoja na Project Zawadi ambao wameingia makubaliano ya kutoa mafunzo kwa walimu na wanafunzi kwa kutoa nyenzo bora za mafunzo, Taasisi ya OCODE yenyewe itahusika na kuwafundisha wanafunzi na walimu stadi za maisha ambazo zitaweza kuwasaidia katika maisha ya kila siku.

Taasisi nyingine ni Jenga Hub yenyewe imeingia makubaliano ya kutoa mafunzo ya matumizi sahihi ya teknolojia kwa walimu na wanafunzi, Taasisi ya Foundation for Disabilities Hope itatoa mafunzo ya lugha ya alama kuanzia ngazi ya awali hadi vyuo vya ualimu.

Taasisi nyingine ni Right To Play ambayo itaweka maudhui ya miongozo mbalimbali ya mbinu za kusoma kwa njia ya michezo kidigitali.

Akizungumza  mara baada ya kuweka saini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TET Dk Aneth Komba amesema kuwa, Taasisi ya Elimu Tanzania inathamini mchango wa wadau unaoendelea kutolewa katika kuboresha elimu nchini huku akisisitiza TET itaendelea kutoa ushirikiano katika masuala mbalimbali katika eneo la elimu.

Amesema, makubaliano haya yamekuja wakati muafaka ambapo kumefanyika maboresho ya Sera na Mitaala ya Elimu nchini ambapo kupitia wadau waliongia makubaliano katika kuhakikisha maboresho yaliyofanyika yanatekelezwa.

Kwa upande wa taasisi hizo zilizoingia makubaliano na TET zimeishukuru Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania kwa kuweka mazingira mazuri ya ushirikiano unaotoa nafasi kwa Taasisi zisizo za Serikali kufanya kazi kwa ubora katika kuwahudumia wananchi hasa katika eneo la Elimu.

Habari Zifananazo

13 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button